- KUTAJWA kwa jina la Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein ndani ya msikiti uliopo kwenye Kijiji cha Kangagani, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba kumesabisha vurugu.
Waumini wa walikubaliana kutotaja kabisa jina la Dk. Shein kwenye msikiti huo kutokana na makovu ya kisiasa yaliyotokea kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita lakini mtoa mawaidha wa msikiti huo kwenye swala ya Ijumaa iliyopita alitaja jina hilo.
Mzozo ulianza baada ya jina la Dk. Shein kutajwa ndani ya msikiti huo huku waumini wakionesha kukerwa kwa mtoa mawaida huyo, taratibu mzozo ukaanza kuibuka.
Hata hivyo, kabla ya vurugu kuwa kuwa, baadhi ya waumini kutokana na kukerwa na jina la Dk. Shein ndani ya msikiti huo, waliamua kutoka nje.
Ilipofika usiku wa saa tatu, Jeshi la Polisi lilivamia msikiti huo uliogomea kutajwa jina la Dk. Shein na kuanza kupiga mabomu.
Mtoa taarifa anasema, baada ya polisi kuvamia na kupiga mabomu, hali ya taharuki ilitanda na kusababisha watu wanaoishi jirani na msikiti huo kuanza kukimbia.
Kuzuka kwa vurugu hizo msikitini kunathibitishwa na Haji Khamisi Haji, Kamanda wa Polisi wa Mkoa ambaye alisema, aliwatuma vijana wake usiku kwa ajili ya kutuliza hali ya sintofahamu kwenye msikiti huo.Amesema kuwa, hatua hiyo ilitokana na baadhi ya waumini wa kutaka kuuchoma moto msikiti huo kutokana na mgogoro huo. Hata hivyo alieleza kutokuwa na taarifa za polisi kupigwa mabomu.
Ndani ya msikiti huo kumegawika pande mbili; mmoja unaunga mkono kutajwa jina la Dk. Shein huku lingine likipiga marufuku jina hilo.
Said Ahmad Muhammad, Ofisa wa Ofisi ya Mufti wa Taasisi ya Kiislam anayeshughulikia Fatwa (maamuzi) amesema, kuwa mgogoro kwenye msikiti huo anaujua.
Na kwamba, pande hizo zilieleza umuhimu wa kutuingiza masuala ya kisiasa kwenye nyumba za ibada.
Hata hivyo, baada ya pande hizo mbili kuelezwa umuhimu wa kutenganisha siasa na ibada, walikubaliana kuwa Dk. Shein hatotajwa tena kwenye msikiti huo na kuwa, ameshangaa jina hilo kutajwa kinyume na makubaliano.
No comments :
Post a Comment