dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, December 19, 2016

HATIMAYE: Mmiliki wa Jamii Forums Atoka Selo Baada ya Kupatiwa Dhamana leo!


BAADA ya kusota kwa wiki moja mahabusu Maxence Melo, Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa Jamii Forums leo ameachiwa   kwa dhamana  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es salaam.

Awali tarehe 16 Disemba alipopandishwa kizimbani kwa mara ya na kusomewa kesi tatu tofauti na kwamba Melo alikosa dhamana kwa sababu ya kutokamilisha mashart ya dhamana.

Mapema leo Mbele ya hakimu  Godfrey Mwambapa Melo amekamilisha mashart ya dhamana

Baada ya kudhaminiwa na wadhamini wawili waliosaini hati ya Sh.5 milioni kila mmoja.

Melo ameshitakiwa kwa kesi tatu ambazo alisomewa mbele ya mahakimu watatu tofauti.

Alianza kwa kushitakiwa katika kesi Na. 456 yenye shtaka moja alilosomewa mbele ya Thomas Simba, Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo ambapo alidaiwa kuzuia taarifa za upelelezi wa jeshi la Polisi.Melo alidaiwa kuwa kati ya tarehe Mosi Aprili na tarehe 13 Desemba, 2016 huko Mikocheni, Kinondoni jijini Dar es Salaam Mkurugenzi huyo wa kampuni ya Jamii media inayoendesha mtandao wa Jamii forums alikataa kutoa taarifa za kiuchunguzi kwa Jeshi la Polisi zilizochapishwa kwenye mtandao huo.

Kesi nyingine ya pili imepewa Na. 457 ikiwa imesomwa mbele ya Hakimu Godfrey Mwambapa, ambapo Melo anadaiwa kati ya tarehe 10 Mei na tarehe 13 Desemba 2016 akiwa Mikocheni Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam alikwamisha kazi ya Jeshi la Polisi kwa kutotoa taarifa za kiupelelezi kwa jeshi la polisi.

Kesi ya tatu kwa Melo ni Na. 458 iliyosomwa mbele ya Hakimu Victoria Nongwa, ambapo wakili wa Serikali Mohammed Salim alidai kuwa Melo alikuwa anamiliki mtandao wa bila ya kusajiliwa hapa nchini Tanzaniana kuwepewa msimbo wa (.co.tz), ikiwa ni kinyume cha sheria.

Anadaiwa kuwa kati ya tarehe 9 Desemba, 2011 mpaka tarehe 13 Desemba, 2016 akiwa kama Mkurugenzi wa Jamii media alikuwa anamiliki mtandao wa Jamii Forum bila kusajiliwa nchini Tanzania.

Kesi hiyo itatajwa tena Desemba 29 mwaka huu.

No comments :

Post a Comment