WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amefika mkoani Mara kwa ajili ya kuendelea na ziara yake ya kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa migogoro ya ardhi nchini.
Lukuvi leo anatarajiwa kutatua migogoro ya ardhi ya wilaya ya Musoma mkoani Mara na kesho atashughulikia migogoro wilaya ya Bunda mkoani humo.
Katika ziara hiyo, Lukuvi atakutana na wananchi wa Musoma mjini na wa Bunda walio na kero za migogoro ya ardhi na kuzitatua pamoja na kutembelea miradi inayosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika wilaya ya Musoma.
Akimaliza Mara ataelekea Arusha ambapo pia atatua migogoro ya ardhi inayoukabili mkoa huo.Juzi akihitimisha ziara yake, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema atamtuma Waziri Lukuvi kushughulikia migogoro katika mkoa wa Arusha ikiwemo katika Wilaya ya Arumeru.
Kwa mwezi huu, Lukuvi ameshatatua migogoro ya ardhi ya mkoa wa Kigoma na wilaya za Kigoma, Kasulu na Kibondo na katika Mkoa wa Shinyanga na wilaya za Kishapu na Shinyanga na mkoani Geita amefanya ziara wilayani Chato.

No comments :
Post a Comment