Hayo yamesemwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alipojibu maswali ya waandishi wa habari baada ya kufungua semina kuhusu jukumu la vyombo vya habari katika kutoa elimu ya sheria, kanuni na utaratibu wa utawala wa ardhi ili kusaidia kutatua migogoro ya rasilimali hiyo.
Amesema kama kuna mtu anafahamu kuna kigogo anayemiliki ardhi na haijaendelezwa ampe taarifa ili afuatilie na kuchukua hatua.
Waziri huyo amesema kuanzia mwakani wale ambao wana mashamba makubwa watawekewa kodi kubwa kwa kuwa hawayaendelezi.Pia, Lukuvi amezionya benki ambazo zimekuwa zikitoa mikopo kwa kutumia dhamana ya mashamba kuwa makini na watu wanaokopa fedha hizo ili ziende kufanya kazi iliyokusudiwa na si vinginevyo.
“Kama mtu anakopa kwa ajili ya kilimo basi wafuatilie kama alichokopea kinafanyiwa kazi,” amesema Lukuvi.
Amesema kuwa tayari wameanza kuyachukua mashamba makubwa ambayo hayajaendelezwa na wamiliki wake na kuwagawia wananchi.
“Hapa Morogoro tutayafuta mashamba makubwa 15 kwa kuwa hayajaendelezwa, hivyo yatasaidia kupunguza migogoro ya ardhi katika mkoa huu,” amesema.
Tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, Wizara ya Ardhi imekuwa ikifuta miliki za mashamba makubwa ambayo hayajaendelezwa kwenye mikoa mbalimbali nchini.
No comments :
Post a Comment