Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(aliyevaa kaunda suti) akitoka ndani ya Kituo cha Polisi cha Bububu, Unguja, Zanzibar mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kituoni hapo leo. Naibu Waziri huyo alitoa agizo kwa Kamishna Hamdan Omar Makame (hayupo pichani) kuwaondoa haraka wamiliki wa miradi mbalimbali iliyopo eneo la Kituo hicho pamoja na katika maeneo mbalimbali ya Jeshi hilo, Zanzibar.Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauniakizungumza na Maafisa wa Polisi na Askari wa Usalama Barabarani katika Ukumbi wa Jeshi la Polisi wa Bomani, Drill Shed, Unguja, Zanzibar. Masauni alilitaka Jeshi hilo, kuwakamata madereva wa magari pamoja na pikipiki wanaovunja sheria za usalama barabarani pamoja na kuwachukulia hatua kali.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimpa maelekezo Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamad Omar Makame pamoja na Watendaji wengine wa Jeshi hilo, wahakikishe wanawaondoa wamiliki wote wa miradi binafsi katika eneo la Jeshi kwa kuanzia na Kituo cha Polisi Bububu. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza kituoni hapo leo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(aliyevaa Kaunda suti) akionyeshwa na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Bububu, Abdulhalim Ali Haji, mpaka wa Kituo cha Polisi cha Bububu, Unguja, Zanzibar, wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kushtukiza kituoni hapo. Masauni alipiga marufuku miradi binafsi iliyozunguka kituo hicho.
Mkuu wa Trafiki Wilaya ya Mjini, Unguja, Zanzibar, Mohamed Talihata, akimuuliza swali Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) wakati kiongozi huyo alipofanya mazungumzo na Maafisa wa Polisi na Askari wa Usalama Barabarani katika Ukumbi wa Bomani, Drill Shed, Unguja.Masauni alilitaka Jeshi hilo, kuwakamata madereva wa magari pamoja na pikipiki wanaovunja sheria za usalama barabarani pamoja na kuwachukulia hatua kali.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame alipokuwa anatoa taarifa ya Utendaji wa Jeshi la Polisi Zanzibar katika Ukumbi wa Mikutano Makao Makuu ya Jeshi hilo, Zanzibar. Masauni alilitaka Jeshi hilo liweke mikakati imara ya kupambana unyanyasaji wa kijinsia ambao umeshika kasi Zanzibar. Naibu Waziri huyo pia alifanya ziara ya kushtukiza katika Kituo cha Polisi cha Bububu na alitoa maelekezo kwa uongozi wa Jeshi hilo, kuhakikisha wanaondoa miradi binafsi iliyopo katika eneo la Kituo hicho.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia), akimsikiliza Kamanda wa Polisi wa Usalama Barabarani, Zanzibar, Kamishna Msaidizi, Mkadam Khamis alipokuwa anatoa taarifa ya Usalama Barabarani katika kikao kilichowashirikisha Maafisa wa Jeshi hilo pamoja na Askari wa Usalama Barabarani, kilichofanyika katika Ukumbi wa Bomani, Drill Shed, Zanzibar. Masauni aliwataka askari hao kuwakamata madereva wote wanaovunja sheria za barabarani na kuwachukulia hatua kali.
/ZanziNews.
No comments :
Post a Comment