Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Mama Tundu amempa mumewe kichapo na kumjeruhi usoni akimtuhumu kutoacha matumizi ya nyumbani.
Tukio hilo lililovuta umati wa watu lililitokea jana saa 2:00 asubuhi mtaa wa Msaranga Wilaya ya Moshi, baada ya mwanamke huyo kumtuhumu mumewe, Fredrick Masawe kutotoa fedha za matumizi.
”Nimechoka na tabia yake ya kunywa pombe kila wakati wakati sisi tunalala njaa kisa eti fedha zote anatumia baa na wanawake wake, siwezi vumilia leo mpaka kieleweke,'' alidai mwanamke huyo.
Akizungumza na gazeti hili baada ya kuamuliwa, mumewe alikanusha kuwa na wanawake bali mara nyingi huwa na marafiki wanaofanya kazi pamoja na kwamba pombe hizo hununuliwa na marafiki zake.
No comments :
Post a Comment