Meneja wa mradi mkubwa wa umeme wa Backbone, Mhandisi Khalid Reuben James, akitoa maelezo kwa wahariri (jawapo pichani), walipotebelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Tagamenda kilichoko nje kidogo ya mji wa Iringa, wakati wa ziara ya wahariri kukagua ujenzi wa mradi wa Backbone unaotoka mkoani Iringa hadi Shinyanga kupitia mikoa ya Dodoma na Singida, Desemba 19, 2016
Wahariri wakitembelea mitambo ya umeme kituo cha Tagamenda
Mhandisi huyu wa Tanesco, akitumia ramani ya mradi huo kuwaelimisha wahariri ukubwa wa mradi huo
Wahariri wakiangalia nguzo zinazobeba nyaya (conductors), za mradi wa Backbone, kwenye kituo cha Tagamenda.
Mhariri wa Business Times, Imma Mbuguni, akipita kwenye moja ya mnara mkubwa wa kupitisha umeme wa msongo wa kilovolti 400 kwenye bwawa la Mtera, mpakani mwa mikoa ya Iringa na Dodoma Desemba 19, 2016
Hii ni moja ya nyumba za askari polisi kituo cha polisi mtera, ambayo TANESCO walilipa mfidia kwa mmiliki wa nyumba hiyo ili kupisha mradi na kumjengea nyumba nyingine mita inayoonekana kipande kushoto
Nyumba mpya iliyojengwa na TANESCO kama fidia kwa mmiliki wa nyumba ya awali aliyepisha mradi huo
Bwawa la kufua umeme la Mtera lililoko mpakani mwa mikoa ya Iringa na Dodoma
Wahariri wakipatiamaelezo ya kiufundi kuhusiana na mradi huo kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Taganenda
Wahariri wakitembelea chumba cha kudhibiti mifumo ya umeme kwenye kituo cha Taganenda mkoani Iringa
Mhandisi James, akiongozana na baadhi ya wahariri na maafisa uhuisno wa TANESCO baada ya kutembelea bwawa la kufua umeme la Mtera
Mhandisi James, akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mradi wa Backbone
Mhandisi James, (aliyevaa kkikoti akisi), akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mradi wa Backbone
NA K-VIS BLOG, Iringa
MRADI wa umeme wa Backbone wa ujenzi wa njia kuu ya umeme ya msongo wa Kilovolti 400 ya urefu wa Kilomita 670 kutoka Iringa hadi Shinyanga kupitia mikoa ya Dodoma na Singida, umekamilika kwa asilimia 100, Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Khalid Reuben James amewaambia wahariri wa vyombo vya habari mjini Iringa leo Desemba 19, 2016.
Pia mradi huo unaohusisha kukamilika kwa upanuzi wa vituo vine vya kupoza na kusambaza umeme kwenye mikoa ya Iringa, Dodoma, Singida na Shinyanga utawezesha kuvipatia umeme vijiji takriban 121, vinavyopitiwa na mradi huo, alisema Mhandisi James.
“Mradi huu ni wa muhimu sana kwenye gridi ya taifa kwa sababu utaongeza uwezo wa kusafirisha umeme kutoka kanda ya Kusini Magharibi, ambako kuna vyanzo vingi vya umeme na kupeleka Kanda ya Kaskazini Magharibi ambako kuna shughuli nyingi za kiuchumi ikiwemo migodi ya madini.” Alifafanua Mhandisi James.
Kwa mujibu wa Mhandisi huyo, mradi huo ulianza mwaka 2013, na ulikadiriwa kugharimu kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 470, ambazo zimetolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na wafadhili wakiwemo, Benki ya Dunia, dola za Kimarekani, milioni 150, Benki ya Maendeleo ya Afrika, (AfDB), na Shirika la Maendeleo la Kijapani, (JICA), Dola za Kimarekani milioni 129.7, Benki ya Uwekezaji ya nchi za Jumuiya ya Ulaya, (EIB), Dola za Kimarekani milioni, 134.5, Shirika la Kiuchumi la Maendeleo ya Korea ya Kusini, (EDCF), Dola za Kimarekani milioni 36.416, na Serikali ya Norway, Sweden na Tanzania, kupitia kwa wakala wa Nishati Vijijini (REA), Dola za Kimarekani milioni 33.4.
“ Ndugu zangu, mradi huu unatoa hakikisho kwa serikali kuwa mipango yake ya kujenga uchumi wa viwanda unawekana pasina shaka, kwani mradi huo mkubwa, utawezesha sasa, kuwapatia wateja umeme ulio bora na wa uhakika,” alsiema.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini, wako kwenye ziara ya kutembelea mradi huo ambao unatarajiwa kuzinduliwa rasmi mapema mwezi Januari, 2017.
No comments :
Post a Comment