Dalili hizo zimeanza kuonekana kwenye kuwania nafasi za uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata ya Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro, ambavyo vyama sita ikiwemo Chadema na CUF kila kimoja kusimamisha mgombea wake. Uchaguzi utafanyika Januari 22 mwakani.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Kata hiyo, Abuu Rashid Liwangile akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana alisema wagombea wa vyama sita vya siasa walichukua fomu na kurejesha.Wote wamepitishwa na tayari wameanza kampeni za uchaguzi huo tangu juzi. Alitaja vyama na wagombea waliopitishwa kuwa ni Chama Cha Mapinduzi (CCM) mgombea wake ni Isihaka Sengo, wakati CUF mgombea wake ni Abeid Mlapakolo.
Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 , Mlapakolo aliwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Morogoro Mjini na alishindwa na mgombea wa CCM, Abdulaziz Abood.
Mlapakolo alijaribu tena kuwania ubunge Jimbo la Kilosa kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015 kupitia mwavuli wa Ukawa, lakini akawekewa mgombea mwenza kutoka Chadema, hivyo kushindwa dhidi ya mgombea wa CCM. Mgombea wa Chadema ni Salum Milindi, wakati TLP imemsimamisha Julius Msilanga.
Chama cha ACT- Wazalendo kimemsimamisha Rahim Elias na Sauti ya Umma (SAU) mgombea ni Mussa Kimonje.
Uchaguzi huo mdogo katika Kata ya Kiwanja cha Ndege, unafanyika baada ya kutokea kifo cha ghalfa cha diwani wa kata hiyo kupitia CCM , Godfrey Mkondya, miezi michache baada ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.
Mbali na Kiwanja cha Ndege, uchaguzi mdogo wa udiwani pia utafanyika katika kata zingine 21 nchini, ambazo ni Ihumwa na Ng’ambi mkoani Dodoma, Igombavanu na Ikweha mkoa wa Iringa, Ngarenanyuki huko Arusha, Kijichi jijini Dar es Salaam, Kinampundu mkoani Singida, Isagehe mkoa wa Shinyanga, Kasansa huko Katavi, Malya mkoa wa Mwanza, Maguu huko Ruvuma.
Kata zingine ni Kimwani mkoa wa Kagera, Nkome mkoani Geita, Lembeni mkoa wa Kilimanjaro, Duru mkoa wa Manyara, Misugusugu mkoani Pwani na Mateves mkoa wa Arusha.
/HABARI LEO
No comments :
Post a Comment