Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Ilemela, Angelina Mabula
Takribani kaya 32 wilayani Ilemela jijini Mwanza zimepaza sauti kwa serikali baada ya kuporwa ardhi yenye viwanja 10 na baadhi ya vigogo huku serikali ikilifumbia macho jambo hilo.
Wanachi hao wamesema mnamo mwaka 2002 watu kutoka halmashauri ya Ilemela walikwenda kwa ajili ya kupima na kuthaminisha makazi,lakini mwaka 2003 waliziwekea lama ya X nyumba zao na kuambiwa kuwa eneo hilo ni la barabara huku wakiahidiwa kuwa nyumba hizo hazitavunjwa mpaka watakapolipwa fidia.
Deogratius Soteli mmoja kati ya wahanga amesema baada ya viwanja hivyo kupimwa bila wao kushirikishwa amedai kuwa walishangazwa kuona maeneo yao yakiuzwa kwa viongozi wa serikali pamoja na vigogo huku familia zikiwa hazijapewa fidia ya aina yoyote wala mahali pakuishi.Amesema pamoja na juhudi za kutaka kuirudisha ardhi hiyo bado hakuna ushirikianao wowote wanaopewa na sekta husika pale wanapofuatilia jambo hilo badala yake huzungushwa hivyo kupelekea kukata tamaa.
John Mongella - Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Aidha wananchi hao wamesema pamoja na vigogo hao kumiliki viwanja hivyo bado eneo hilo halijaendelezwa na hakuna mtu aliyefidiwa eneo wala mali zao hivyo wanamuomba Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi kuingilia kati ili wapate haki zao.
Baada ya malalamiko hayo kituo hiki kilimtafuta mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Ilemela John Wanga hili kutoa ufafanuzi wa jambo hilo ambapo amesema yeye kama mkurugenzi hajawahi kupata malalamiko yoyote kutoka kwa wananchi juu ya mgogoro huo wa ardhi hivyo amewataka wananchi hao kufika ofisini kwake ili kupata muafaka wa jambo hilo.
Wanaotuhumiwa katika sakata hilo ni John Mongela (mkuu wa mkoa wa mwanza) Anna Makinda, Anna Abdalah, Lameck Airo, na Anthony Diaro.
Source: EATV
No comments :
Post a Comment