Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, December 21, 2016

Kuwait kuipa Tanzania Sh 74 bilioni za barabara Kuwait kuipa Tanzania Sh 74 bilioni za barabara!



Dar es Salaam. Serikali ya Kuwait imeahidi kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa zaidi ya Sh 74.8 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa barabara yenye urefu wa Kilometa 85 kwa kiwango cha lami kutoka eneo la Chaya hadi Nyahua mkoani Tabora.

Ahadi hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na mwakilishi wa Balozi wa Kuwait hapa nchini, Mohammad Alamiri, aliyeongoza ujumbe kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait, ulipomtembelea na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, ambapo wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya Tanzania na Kuwait.

Dk Mpango ameushukuru Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait (Kuwait Fund) kwa kuipatia Tanzania mkopo huo wenye masharti nafuu utakaochochea maendeleo kwa Watanzania hususani wanaoishi katika maeneo ambayo barabara itajengwa kwa kuwa watarahisishiwa usafiri na usafirishaji wa bidhaa zao hivyo kukuza uchumi wao binafsi na Taifa kwa ujumla.

“Riba waliyoiweka mezani kwa mazungumzo ni asilimia 2 lakini nimewaomba waangalie uwezekano wa kuiteremsha walau ifike asilimia 1.5 na wamependekeza kipindi cha kuanza kulipa mkopo kiwe miaka ishirini ijayo lakini nimewaomba wasogeze hadi kufikia miaka 25 kama ilivyo kwa mradi wa Hospitali ya Mnazimmoja” aliongeza Dk Mpango.

No comments :

Post a Comment