Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Theophil Makunga (kulia), akizungumza Dar es Salaam leo wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa wahariri kupitia sheria ya huduma ya vyombo vya habari uliyopitishwa na Bunge pamoja na kujadili mpango mkakati wa TEF wa kuendeleza tasnia ya habari nchini. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Habari Tanzania (TMF), Ernest Sungura.
Mtaalamu Mshauri Rosemary Mwakitwange akiongoza mkutano huo.
Mwakilishi kutoka Jukwaa la Wahariri la Afrika Kusini akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Theophil Makunga (kulia) na Mtaalamu Mshauri Rosemary Mwakitwange wakiangalia mada zitakazo jadiriwa katika mkutano huo.
Wahariri Idrisa Jabir na Charles Mwankenja (kulia), wakijadili jambo.
Wahariri kutoka kushoto, Joseph Kulangwa, Abdallah Majura na Ibrahim Issa ambaye ni mjumbe wa TEF wakifurahia jambo kwenye mkutano huo.
Wahariri wakifurahia jambo.
Wahariri wakiwa kwenye mkutano huo.
Wahariri, Joseph Kulangwa na Abdallah Majura wakipitia mada zitakazo jadiliwa.
Wahariri, Shermax Ngahemera (kushoto), Julian Msacky na Flora Wingia (kulia), wakifuatilia mada za mkutano huo.
Taswira ndani ya ukumbi wa mkutano huo
Wahariri ndani ya chumba cha mkutano.
Na Dotto Mwaibale
WAHARIRI wa vyombo vya habari wamekutana katika mkutano maalumu wa siku mbili kwa ajili ya kujadili mambo kadhaa yanayohusu tasnia hiyo nchini.
Akizungumza wakati akifungua mkutano huo Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Theophil Makunga alisema mkutano huo utawajumuisha wadau wa sekta ya habari kutoka ndani na nje ya nchi.
"Tumewaalika wenzetu wa nje ili watupe uzoefu wa jinsi wanavyofanya katika tasnia ya habari katika nchi zao" alisema Makunga.
Alisema katika mkutano huo ambao unafanyika Hoteli ya Protea Court Yard mambo yatakayo zungumziwa ni kupitia sheria ya huduma ya vyombo vya habari iliyopitishwa na Bunge na kusainiwa na Rais Dk. John Magufuli pamoja na kujadili mpango mkakati wa Jukwa la Wahariri wa kuendeleza tasnia ya habari nchini.
No comments :
Post a Comment