Idd Amin aliyekua Rais wa Uganda
Wakati huo ARAB WORLD ilikuwa inauguza vidonga vya kushindwa na ISRAEL katika vita vya siku 6 ambavyo ISRAEL ilionyesha UBABE wake katika MEDANI ya vita vya ardhini,angani na Majini.Gaddafi na Maofisa wengine vijana walikuwa madarakani wakati huo waliweza kwa kiasi fulani kuondoa unyonge huo katika nchi za Kiarabu.
Mwaka 1972 March Gaddafi alianza kufanya Mazungumzo ya siri na IDD AMIN na alimwomba avunje Mahusiano ya Kibalozi na ISRAEL na yeye GADDAFI angeweza kumpa misaada yoyote ya kijeshi na misaada mingine ya ki-uchumi na IDD AMIN alikubaliana naye na hapo hapo Balozi wa ISRAEL nchini Uganda alifukuzwa na kurudi kwao yeye pamoja na washauri wa mambo ya kijeshi wote hapo hapo GADDAFI alitoa 5,000,000USD.
Hapo GADDAFI alipata sifa sana katika nchi za Kiarabu maana aliweza kukatilia Mbali Uhusiano wa Uganda na Israel na hapo hapo Libya ilianza kuweka Vitega uchumi vyake nchini Uganda.
IDD AMIN alilengwa sana na GADDAFI sababu yeye alikuwa Mwislamu na istoshe yeye alikuwa kama mtu mbabe sana na aliyefundishwa vizuri na ISRAEL hivyo ingekuwa tishio sana kwa nchi za Kiarabu ndiyo maana Gaddafi alimushawishi AMIN aunge mkono harakati za nchi za Kiarabu hasa kuhusu PALESTINA na alipokubali alizawadiwa zawadi nzuri pamoja na pesa ili kuinua uchumi wa UGANDA. Misaada hiyo aliahidiwa haiwezi kukoma mpaka mwisho wa utawala wake ndiyo maana hata Utawala wake ulipowekewa vikwazo na OAU wakati ule 1975 pamoja na nchi za magharibi kumwekea vikwazo lakini LIBYA na SAUD ARABIA waliendelea kumwaga misaada UGANDA na walilipa michango yote ya UGANDA huko OAU mwaka 1975.
Uhusiano kati ya Tanzania na Uganda uliendelea kuzorota baada tu ya IDD AMIN kumpindua MILTON OBOTE Mwaka 1971,Baada ya Mapinduzi hayo Rais Nyerere alimpa hifadhi ya kisiasa MILTON OBOTE pamoja na wakimbizi wengine 20,000 waliokimbia Utawala wa mabavu wa IDD AMIN,Baadaye mwaka 1972 wakimbizi wa Uganda walifanya jaribio lililoshindwa la kutaka kumpindua AMIN tokea Tanzania,Kitendo hicho kilimfanya AMIN alimshutumu sana Nyerere kuwa nyuma ya tukio hilo la kuwapatia silaha wafuasi wa MILTON OBOTE tokea hapo uhusiano wa Tanzania na Uganda ulizidi kuwa tete sana
Hatimaye Mwaka 1978 wapinzani wa IDD AMIN walivamia Ikulu ya Kampala lakini IDD AMIN aliweza kutoroka na Helicopter hii ilikuwa kipindi kigumu sana kwa IDD AMIN hasa alikosa maelewano na Makamu wake wa Rais wakati ule aliyekuwa anaitwa General MUSTAFA ADRISA aliyepata ajali kwa ajali ambayo ilihisiwa kuwa ilikuwa ya kupangwa na wale askari waliokuwa wanamuunga mkono walimuasi AMIN hivyo kupelekea askari hao kuvamia Ikulu ya Kampala,
Kitendo hicho kilimfanya AMIN Kutuma askari wake watiifu kwenye kambi iliyokuwa inajulikana kama SIMBA BATTALION na kusababisha waasi kukimbilia Tanzania ambako kulikuwa na askari wenzao kutoka Uganda waliokuwa wakimpinga AMIN Kitendo ambacho AMIN kilimfanya awafuatilie huko waliko kwa matamushi yake mwenyewe alitumia dakika 25 tu kuteka eneo lote la kagera na kulitangaza eneo hilo kuwa sehemu ya UGANDA.
Katika uvamizi huo ambao ulihusisha zaidi ya askari 3,000 wenye silaha za kisasa wakti huo,Majeshi ya Uganda yaliyokuwa hayana Nidhamu walianza kwa Kuwabaka wanawake na walipora vitu mbali mbali vijiji viliteketezwa Makanisa yaliharibiwa vilevile waliweza kupora mashine nzito,Mabati,Magari,Mabomba pia yaliharibiwa shule pamoja na Hospitali hazikuweza kubaki salama mbele ya askari wa Amin,Miji jirani na Bukoba ilifulika wakimbizi waliokuwa wakikimbia toka uwanja wa mapambano ambao AMIN alisema aliweza kukalia eneo hilo kwa mwendo wa SUPERSONIC yaani dakika 25 tu na kilifanya eneo la UGANDA. ndipo Majeshi ya Tanzania yalipoingia vitani na ukawa ndio mwanzo wa VITA VYA KAGERA
No comments :
Post a Comment