Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, January 29, 2017

Mzee Mwinyi aonya uvunjifu wa amani!


Ikungi. Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amewataka Watanzania wasiruhusu upungufu wa ubinadamu kuwa chanzo cha kuhatarisha amani na utulivu unaotamalaki nchini.

Mzee Mwinyi alitoa wito huo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati ufunguzi wa Msikiti Qadiriyya katika Kijiji cha Ititi, Wilaya ya Ikungi mkoani Singida ambao umegharimu Sh54 milioni.

Alisema Mungu ameumba binadamu ambao siyo malaika, hivyo kuhitilafiana ni jambo la kawaida na haliepukiki.

“Hatuwezi kuzikubali hitilafu hizi, lakini hatuwezi kuzikataa kwa sababu zitakuwapo tu upende usipende. Tunachopaswa kufanya ni kutoziruhusu kutumiliki, binadamu ndiyo tuzimiki. Kwa njia hiyo amani na utulivu utaendelea kudumu nchini,” alisema.Alisema ili hitilafu hizo zisisababishe ugomvi au vurugu zitakazochangia kutoweka kwa amani na utulivu, Watanzania wanatakiwa kupendana kwa dhati na kuvumiliana. “Inapotokea bahati mbaya tukahitalifiana, isiwe sababu ya kugombana… hitilafu husika itafutiwe ufumbuzi kwa amani. Kwa ujumla kila mtu ashike yake yaliyo halali yakiwamo ya dini, ugomvi wa nini?” alihoji Mzee Mwinyi.

Alisisitiza kwamba Watanzania waendelee kudumisha utamaduni kwa kuombana radhi zinapobainika dalili ugomvi, au hitilafu.

Akitoa salamu zake, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Rehema Nchimbi aliahidi Serikali kuendelea kushirikiana kwa ukaribu na dini zote katika kuhudumia wananchi kwa ajili ya maendeleo.

No comments :

Post a Comment