Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Mwanajuma Majid Abdalla akimuapisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Kusini Pemba Ndg Yussuf Mohammed Ali hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Afisi ya Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba akichukua nafasi ya Afisa Tawala aliyepita Ndg Ahmed Khalid Abdalla amehamishiwa Mkoa wa Kaskazini Pemba
Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla, akizungumza jambo katika hafla ya makabidhiano baina ya Katibu Tawala wa mkoa wa Kusini na Kaskazini ambao wamebadilishwa vituo vya kazi.
Makatibu hao wakikabidhiana majukumu huko katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, wakati Mkuu wa mkoa huo akishuhudia.
Mkuu wa Wilaya ya Mkoani, Hemed Suleiman Abdalla, akizungumza mara baada ya kumalizika hafla ya makabidhiano ya majukumu baina ya Katibu Tawala wa Mkoa Kusini na Kaskazin
Naibu Waziri Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalumu , Shamata Shaame Khamis, akizungumza na Maofisa na Wafanyakazi wa Baraza la Mji Chakechake Pemba wakati wa ziara yake kisiwani huo kuangalia utendaji wa Wizara yake.
Wafanyakazi wa Baraza la Mji Chake Chake ,wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala Za Mikoa na Idara Maalumu, Shamata Shaame Khamis , wakati akizungumza nao huko katika Ofisi ya Baraza hilo Chake Chake-Pemba.(Picha na Hanifa Salim -Pemba.
No comments :
Post a Comment