Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, February 25, 2017

DAR ES SALAAM AND THE POLITICS OF A SLAUGHTERHOUSE (ABATTOIR)!

Baada ya Wema Kumwaga Ugali, Steve Nyerere Amwaga Mboga, Afunguka Mazito!

Mwigizaji na mchekeshaji mahiri Bongo, Steven Mengere 'Steve Nyerere', amefanya mkutano na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Millenium Tower, Makumbusho jijini dar es Salaam ambapo amekiri kwamba sauti iliyokuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii, kweli ni yake na alikuwa akizungumza kwa simu na mama mzazi wa Wema Sepetu, Miriam Sepetu. Steve Nyerere amesema kwamba ndani ya video hiyo, yote yaliyokuwa yakisikika, ikiwemo yeye kutamba kwamba amezungumza na viongozi na mawaziri wa serikali, hayakuwa ya kweli bali ilikuwa ni kwa lengo la kumlainisha mama Wema ili atulie.Steve ametumia nafasi hiyo kuomba msamaha kwa Rais John Magufuli kwa kuwataja mawaziri wake kwenye video hiyo, pia amewaomba radhi mawaziri wote waliotajwa kwenye video hiyo pamoja na Chama cha Mapinduzi kwa yote yaliyotokea na ameahidi kwamba kamwe hataihama CCM. Hayo yamekuja siku chache baada ya sauti kuzagaa mitandaoni, Steve Nyerere akisikika akizungumza na mama Wema, akieleza jinsi alivyowashawishi wabunge waijadili ishu ya Wema kukamatwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za matumizi ya madawa ya kulevya, na kumtuhumu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwamba anamuonea Wema.

No comments :

Post a Comment