Ni shirika ambalo mambo yake ni siri kuu. Mimi nilifanya utafiki kwenye mitandao, nikafatilia historia yao kama inavyoonyeshwa mara kwa mara kwenye makala za historia katika televisheni za magharibi pamoja na kuongea na watu waliofuatilia kwa karibu mambo yao.
Kwenye maelezo yao kwa nje Free masons wanajitangaza kama shirika zuri tu.
Naomba niorodheshe mambo machache niliyoambiwa kuhusiana na Freemasonry:
Kwenye maelezo yao kwa nje Free masons wanajitangaza kama shirika zuri tu.
Naomba niorodheshe mambo machache niliyoambiwa kuhusiana na Freemasonry:
1. Ni kweli Freemasonry kama ilivyo maana yake kwanza ilkuwa ni kundi la mafundi waashi (masons) au wajenzi kuwa lugha nyingine. Walikuwa ni wataalamu waliobobea kwenye masuala ya ujenzi wa mahekalu na mabenki ya zama hizo zinazoitwa kwa kizungu (medieval times).
Niliambiwa walikuwa ni watunzaji wa pesa za kanisa katoliki. Kwani walikuwa wanajenga mahekalu(cathedrals) za wakatoliki na mabenki/ mahandaki ya kuhifadhia pesa pamoja na kuzikia(catacombs).
Niliambiwa wanaweza kujenga hayo maandaki kwa utaalamu mkubwa kiasi kwamba ukiingia ndani ya hayo mahandaki bila ramani unaweza ukashindwa kutoka hata unaweza kupotelea humo humo ndani usiweze kutoka tena. Hicho ndicho kilichokuwa ni kiwango cha utaalamu wao.
2. Kwa kuwa walikuwa ni waashi ndiyo maana alama zao ni vifaa vya ujenzi, Pima maji n.k
3. Inasemekana mji mkuu wa marekani (Washington DC) ulisanifiwa na kujengwa na Freemasons. Na inasemekana ni mji makini ambao umejengwa ukizingatia pembe tatu zenye nyuzi zinazowakilisha u freemason.
4. Ikatokea kipindi ambapo hawa freemasons wakaasi kwa kuanza kujishirikisha na mambo ya nguvu za giza. Wengine wanasema walianza kuiba pesa za kanisa katoliki, lakini ukweli halisi haujulikani. Kutokana na sababu hizi na zinginezo ambazo ni siri kati ya kanisa katoliki na freemasons, Freemasons wakafukuzwa kutoka ukatoliki.
Ndio maana hakuna maelewano kati ya freemasons na wakatoliki. Wakatoliki wakaanzisha shirika jingine badala ya hao freemasons lijulikanalo kama Jesuits.
Jesuit Fathers ni mapadri wa katoliki wa daraja la juu sana wenye elimu ya juu zaidi ambao hufanya kazi za siri za utawala na udhibiti ndani ya kanisa katoliki.
5. Kuhusu imani yao (freemasons) nikaelezwa kwa kifupi kuwa wanaamini Yesu na Lucifer ni mtu na ndugu yake. wanaamini kuwa Lucifer ndiye mwema na mzuri lakini wanaamini kuwa Yesu ndiye mwenye mabaya. alimfanyia hila Lucifer aonekane mbaya.
6. Kinachoendelea ndani yake kuhusiana na ibada zake ni siri kwani kuna daraja ambazo muumini wa freemason anapanda kutokana na kubobea katika imani ikiwa ni pamoja na kutunza siri zao. Ninajua kuwa daraja ya juu kabisa ni nyuzi ya 33 (33rd degree)
7. Ni watu wenye nguvu mno na mambo yao ni makubwa mno na siri zao ni nzito mno. Ndiyo maana haziko wazi.
Wafuasi wa kiwango cha chini wala hawajui shirika hili linahusika na nini manake hata wao hawaambiwi kitu. Kwa wafuasi wa daraja ya chini wanakwenda ku socialize tu. Yaani kwa wasio jua kitu kule kwenye lodge zao ni kama ywca au wmca au club hivi. Kwenye nchi kama marekani watu wasio jua siri wanachukulia kama sehemu za kusocialize tu.
8. Freemasonry inawekwa pamoja na makundi mengine makubwa ya siri, yanayoendesha ulimwengu mzima kwa nguvu za kiuchumi, siasa na mambo ya utawala.
No comments :
Post a Comment