Serikali ya Afrika Kusini imetupilia mbali ombi la Nigeria ya kutaka Muungano wa Afrika AU, kuingilia kati na kuzima mashambulizi yanayowalenga raia wa Nigeria wanaoishi nchini Afrika Kusini.
Mwishoni mwa wiki maduka 30 yanayomilikiwa na raia wa kigeni yaliporwa na kuchomwa mjini Pretoria.
Lakini msemaji wa wizara ya mashauri ya nchi za kigeni Clayson Monyela, aliliambia gazeti la New Age la Afrika Kusini kuwa visa hivyo ni vichache.
Mapema wiki hii mshauri wa rais wa Nigeria alisema watu 116 raia wa Nigeria, wameuawa nchini Afrika Kusini katika kipindi cha miaka mwili.
Wakati huo huo mashirika ya usalama nchini Afrika kusini yamelaani taarifa kwenye mitandao ya kijamii baada ya mashambulizi ya hivi majuzi kwenye mali inayomilikiwa na raia wa kigeni kwenye miji ya Johannesburg na Tshwane.
Serikali inasema imewahakikishia watu wa nchini humo wakiwemo raia wa kigeni kuwa mashirika ya usalama yanaelewa vitisho vinavyosambazawa kwenye mitandao ya kijamii.
Maandamano yanapangwa siku ya Ijumaa mjini Pretoria na raia wa Afrika Kusini wanaowalaumu wageni kwa ulanguzi wa mihadarati na ukahaba.
Pia wanadai kuwa wanapoteza ajira kwa raia wa kigeni.
No comments :
Post a Comment