Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, February 19, 2017

Serikali kugawa vifaranga vya samaki kwa wakulima kuanzia Oktoba!

Image result for FISH FARMING IMAGES

Na Salmin Juma , Pemba
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema inatarajia kugawa vifaranga vya samaki kwa wakulima ifikapo mwezi agosti mwaka huu.

Waziri wa kilimo uvuvi na mifugo Mh Hamad Rashid Moh’d amesema tayari Serikali imeshataayarisha nasari ya mazalio ya vifaranga hao na muda si mrefu vitagawanywa kwa wakulima .

Ameyasema hayo huko Ukumbi wa kilimo Weni Wete katika mazungumzo na wakuu wa mikoa ,wilaya na maafisa wa ulinzi na usalama wakati akielezea fursa za kiuchumi kwa wananchi wa Zanzibar.

Waziri huyo amesema endapo wananchi watachangamkia fursa zilizopo wanaweza kuinua kipato chao cha uchumi kupitia kilimo hicho cha ufugaji wa samaki.

Hamad amedokeza kwamba Vifaranga vya samaki vipatavyo elfu nane tayari vimeshatayarishwa kugaiwa wakulima wa samaki Unguja na Pemba.

No comments :

Post a Comment