Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, February 10, 2017

Uber kutengeza magari yanayoruka!

Magari ya kuruka ya Uber kama yaliovyoelezewa katika mpango wake.

Muhandisi wa zamani wa shirika la maswala ya angani Nasa ameajiriwa na kampuni ya teksi Uber kusaidia katika utafiti wake wa kutengeza magari yanayoruka.

Mark Moore anajiunga na Uber kama mkurugenzi wa uhandisi wa angani.

Lengo la Uber katika kutengeza magari yanayoruka liliangaziwa mwezi Oktoba ambapo maswala ya kupaa na kutua yalijadiliwa.

Uber tayari inawekeza katika magari ya kujiendesha ikishirikiana na kampuni ya Volvo na Daimler.

Katika mipango yake Uber imesema kuwa katika mahitaji ya angani ,kampuni hiyo ina uwezo wa kuimarisha uchukuzi wa mijini na kuwapatia wateja wake muda wanaopoteza kila siku wanaposafiri.



Kampuni ya kutengeza magari ya ya Aeromobil kutoka nchini Slovakia ni miongoni mwa kampuni ambazo zina mpango wa kutengeza gari la kuruk

''Huku majumba marefu yakisaidia katika utumizi mchache wa ardhi, uchukuzi wa mijini utatumia maneeo matatu ya angani kukabiliana na msongamano wa magari ardhini''.



Mpango huo utashirikisha mtandao wa ndege za kielektroniki ambazo zitapaa na kushuka wima.

Moore alifichua mpango kama huo katika jarida lililochapishwa wakati alipokuwa Nasa.

Alisema kuwa mpango wa kutengeza vitu vinavyopaa kielektroniki ni mpango muhimu wa kiteknolojia wa ndege na kuongezea kwamba kitu kinachozuia kuanza kwa mpango huo ni betri zitakazotumika.

Kampuni ya kutengeza magari ya ya Aeromobil kutoka nchini Slovakia ni miongoni mwa kampuni ambazo zina mpango wa kutengeza gari la kuruka ambayo inatarajiwa kuingia katika soko mwaka huu.

No comments :

Post a Comment