Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Sunday, February 26, 2017
Watendaji wa Serikali wadakwa na dawa za kulevya!
Kikosi maalumu cha kudhibiti dawa za kulevya wilaya ya Muleba mkoa wa Kagera kimefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 14 wakiwemo watendaji na wenyeviti wa serikali za vijiji wakilima dawa za kulevya aina ya bangi,ukataji miti ya kupasua mbao, uchomaji mkaa,uwindaji haramu huku wengine wakiojihusisha na uzalishaji wa pombe haramu aina ya gongo kinyume cha sheria za nchi.
Operesheni ya kudhibiti dawa za kulevya,ujangiri,na uhalibifu wa mazingira katika pori la akiba Burigi upande wa Muleba operesheni hiyo imefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wakiwa na nyara za serikali akiwemo mwenyekiti wa kitongoji cha nyantungu kata ya nyakabango bw.athuman kanyamafa aliyekama twa akivuna mbao huku wawindaji haramu wakikamatwa muda mchache baada ya kuuwa mnyama aina ya swala kinyume cha sheria za nchi na walipohojiwa hali ilikuwa hivi.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Muleba mhandisi richard ruyango ambaye anaongoza kikosi kazi cha askari wa jeshi la wananchi,magereza,uhamiaji,polisi kwa kushirikiana na wananchi amesema kuwa hata sita kuwachukulia hatua za kisheria watendaji wa serikali wanaokiuka sheria,taratibu na kanuni za nchi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment