Jumuiya ya Wenye magari ya kubeba mchanga visiwani Zanzibar imesema muda waliopangiwa na Serikali wa kuingia na kutoka katika mashimo ya kuchimbia mchanga utasababisha madereva wengi kupoteza nafasi zao za ajira kutokana na hasara inayopatikana ikiwemo kufanya kazi mara moja kwa siku pamoja na mzigo mkubwa wa kodi unaowakabili.
Akizungumza na waandishi wa habari katika shimo la kuchimbia mchanga liliopo eneo la Bumbwini, Wilaya ya Magharib B, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Msabah Hassan Silima amesema hivi sasa eneo hilo linakabiliwa na msongamano mkubwa wa magari kutokana na utaratibu uliowekwa wa kuingia shimoni kuanzia saa moja za asubuhi na kutoka saa kumi za jioni.
Channel Ten imeshuhudia msongamano mkubwa wa malori yanayobeba mchanga yanayoingia na kutoka katika shimo hilo, ambalo limepangiwa utaratibu wa kutumika kwa siku tano kwa wiki huku magari hayo yakizuiliwa kuondoka au kunyimwa vibali pale inapopindukia muda uliopangwa na Serikali.
Baadhi ya Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maghrib B, wamekiri kuwepo kwa changamoto mbalimbali katika eneo hilo, na kutoa ushauri kwa viongozi wa ngazi za juu wa Serikali kuwashirikisha wadau wote wa sekta hiyo kabla ya kufanya mabadiliko yoyote ya sheria na taratibu za uchimbaji wa mchanga.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema hivi sasa kuna eneo dogo lililobaki kwa ajili ya uchimbaji wa mchanga na rasilimali hiyo italazimika kuagizwa kutoka nje ya visiwani Zanzibar.

No comments :
Post a Comment