zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, March 14, 2017

Hali ya Hospitali ya rufaa Morogoro yamshtua Jaffo!


Naibu Waziri ofisi ya Rais,Tawala za mikoa na serikali za mitaa,TAMISEMI, Suleiman Jaffo,ameeleza kutoridhishwa na hali ya uchakavu wa magodoro,neti na ukosefu wa mashuka ya kulalia katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika hospitali hiyo na kutembelea wadi ya kina mama waliojifungua kwa njia ya upasuaji.

Jaffo aliyewasili katika hospitali hiyo ya rufaa majira ya asubuhi,amefika katika Ofisi ya Mganga mkuu wa mkoa,ambapo pamoja na kupewa taarifa fupi ya maendeleo yanayoendelea kufanyika katika hospitali hiyo na Mganga mkuu wa mkoa Dk Frank Jacob,ikiwemo kuanza kwa matumizi ya Tele Medicine na mikakati ya kubadilisha Xray ya mfumo wa kizamani kuwa katika mfumo wa kisasa,bado akataka kuoneshwa baadhi ya maeneo ikiwemo wadi ya wazazi na majeruhi,na kushangazwa na hali aliyoikuta katika wadi ya wazazi waliojifungua kwa njia ya upasuaji.
Aidha kiongozi huyo ameeleza kushangazwa na kitendo cha mganga mkuu wa Manispaa,Dk Barakael Jonas na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro John mgalula kushindwa kueleza kiasi cha fedha zilizoingia katika awamu ya tatu ya mfuko wa Basket Fund,na kuagiza taarifa zote za ujio wa fedha hizo na matumizi yake ziwasilishwe kwa mkuu wa wilaya ya Morogoro ili aweze kufanya ufuatiliaji wake.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo,kwa mwaka huu Manispaa ya Morogoro pekee imepelekewa shilingi milioni 533 za Basket Fund huku Morogoro vijijini zikipelekwa shilingi milioni 923,na asilimia 30 ya fedha hizo inapaswa kutumika kwa manunuzi ya dawa na vifaa tiba.

No comments :

Post a Comment