Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, March 5, 2017

Rais JPM aagiza Dangote apewe eneo la kuchimba makaa ya mawe!

Rais Magufuli akimaliza matatizo ya Kiwanda cha Dangote Cement Mtwara. Hotuba ya Rais Magufuli kiwanda cha Dangote Mtwara na uzinduzi wa Magari ya Dangote. Rais Magufuli alitoa maelekezo juu ya Matatizo na Malalamiko yote yanayohusiana na kiwanda hicho ikiwemo upatikanaji wa makaa ya mawe na Gas kwa ajili ya matumizi ya kiwanda hicho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Magari makubwa ya kusafirishia Saruji kiwanda hapo. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego.

Rais Dk. John Pombe Magufuli amemuagiza waziri wa nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo kuhakikisha ndani ya siku saba mmliki wa kiwanda cha saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote anapewa eneo la kuchimba makaa ya mawe kwa ajili ya kuendeshea mitambo ya kiwanda chake.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo wakati akizindua magari ya kubeba mizigo ya dangote ambayo yalishushwa hivi karibuni katika bandari ya Mtwara ambapo jumla ya magari 580 yamezinduliwa kwa ajili kusambaza saruji katika miji midogo hapa nchini.

Rais Magufuli ambae amekaribishwa kuhutubia wananchi na kuzindua magari hayo na mmliki wa kiwanda hicho Alhaji Aliko Dangote ,amesema kuwa kuna baadhi ya watu wanakwamisha kiwanda cha dangote kupata makaa ya mawe na kwamba ndani ya siku saba mmliki wa kiwanda hicho anatakiwa awe amepata leseni pamoja na eneo la kuchimba makaa ya mawe.

Katika hatua nyingine ameagiza mamlaka zinazohusika na masuala ya gesi kuuza gesi moja kwa moja kwa mmliki wa kiwanda cha saruji cha dangote bila kupitia kwa mwekezaji mwingine.

Rais Magufuli pia ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha kufua umeme cha Mtwara ambacho kitazalisha umeme kwa ajili ya mikoa ya Lindi na Mtwara ambapo ameagiza wadaiwa sugu wa TANESCO kukatiwa umeme.

No comments :

Post a Comment