Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, March 7, 2017

Si deni, ni Tanesco kuikomoa Zecco!


Na Melisa J
Taarifa kutoka Z’bar zinaeleza kuwa kuchelewa kulipwa kwa deni la umeme hadi kufilia Bilioni 121 kunatokana na Shirika la Umeme la huko (ZECO) kutokubaliaa na gharama za umeme wanazotozwa na TANESCO.

Imeelezwa kwamba sio kweli kwamba ZECO hawataki kulipa deni, isipokua hawataki kulipa kwa viwango vilivyowekwa na TANESCO. Kwa mujibu wa viwango vya gharama za umeme vya TANESCO, ZECO wananunua umeme kwa gharama zilezile ambazo TANESCO wanauza kwa wateja wengine wa bara.

Hoja ya ZECO ni kwamba haiwezekani TANESCO wawauzie umeme kwa viwango wanavyouziwa wateja wengine kwa sababu TANESCO haihusiki na gharama za kuweka miundombinu ya umeme Zbar wala matengenezo yake.


Afisa mmoja wa ZECO niliyezungumza nae kwa simu na hakutaka jina lake liwekwe wazi amesema “Tanesco kutucharge gharama sawa na wateja wengine ni unyonyaji. Kama miundombinu yote tunaweka wenyewe (nguzo, transforma, nyaya, etc), bado mishahara ya wafanyakazi tunalipa wenyewe na gharama za uendeshaji, pia tunafanya maintanance wenyewe, kwanini Tanesco watuuzie umeme sawa na wanavyowauzia wateja wengine?”

Mvutano huo kuhusu bei za umeme ambazo ZECO wanapaswa kulipa TANESCO ndio umesababisha deni hilo kufikia Bilioni 121 kwa sasa.

Juzi akiwa mkoani Mtwara Rais Magufuli aliagiza TANESCO kuwakatia umeme Zanzibar kutokana na kushindwa kulipa deni hilo. Akizungumza alipokwenda kuweka jiwe la msingi kwenye kituo kipya cha Tanesco mkoani Mtwara, Rais Magufuli alikaririwa akisema;

“Msiogope mnapaswa kukata huduma hii kwa taasisi yoyote ambayo hailipi bili zake. Nataka kumwambia waziri Muhongo kwamba umeme unapaswa kukatwa hata Ikulu. Nikilala gizani, maafisa wa Ikulu ambao hawajalipa watawajibika na sio wewe. Una hakikisho langu kwa hili. Ninaambiwa SMZ haijalipa Sh121 billion. Ninyi (Tanesco) sio wanasiasa. Mnapaswa kuzingatia majukumu yenu ya kitaaluma… kata huduma ya umeme. Nimesema kata..”



FB

No comments :

Post a Comment