Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, March 10, 2017

Tundu Lissu, Masha wanunua kesi ya kupinga uchaguzi TLS!


Baadhi ya wagombea wa nafasi ya  urais kupitia kwa chama cha wanasheria wa Tanganyika TLS wanatarajia kuwasilisha maombi ya kujumuishwa kama wadaiwa katika kesi ya kupinga kufanyika kwa uchaguzi wao uliopangwa kufanyika tarehe 18  ya mwezi huu

Wamefikia hatua hiyo ili kuuongezea nguvu upande wa wadaiwa kufuatia kesi iliyofunguliwa na wanachama wawili wa chama hicho ambao wamefungua kesi katika mahakama kuu kupitia mkoa wa Dodoma na Dar es salaamu .

Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo mgombea TUNDU LISSU amesema uchaguzi huo umekuwa ukifuatiliwa kwa karibu na watu wengi huku akibainisha kuwa kuna kile alichokiita njama dhidi ya kuuharibu uchaguzi huo.


Lissu ameongeza kuwa wanachama wa chama hicho hawatakuwa tayari kuona uchaguzi unasitishwa kutokana na sheria za chama hicho kusisitiza kufanyika kwa uchaguzi wa chama hicho ambacho amedai kimekuwa na mchango mkubwa katika tasnia ya sheria nchini.

Katika kesi ya msingi ya kupinga uchaguzi huo iliyofunguliwa na wanachama hao, washtakiwa ni mwanasheria mkuu wa serikali pamoja na chama chenyewe (TLS).

Kwa upande wake mgombea mwingine wa nafasi ya urais ambaye aliwahi kuwa waziri wa mambo ya ndani  mheshimiwa LAWRENCE MASHA amebainisha kuwa chama chao hakina kipengele chochote kinachozuia wanasiasa kugombea nafasi ya uongozi katika chama hicho huku akiwataka wanachama wa chama hicho kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano mkuu wa chama hicho ambao unatarajiwa kufanyika mkaoni Arusha siku ya tarehe 18 ya mwezi huu

No comments :

Post a Comment