Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Tuesday, March 14, 2017
VIDEO: Rais Magufuli ampigia simu Diamond leo March 14, 2017!
Leo March 14 2017 kupitia kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na Clouds TV, Rais Magufuli amepiga simu na kuzungumza na Mwimbaji wa Bongo fleva Diamond Platnumz baada ya kusikia Diamond akimuomba Rais Magufuli aisadie sanaa ya muziki kama anavyosaidia mambo mengine.
>>>”Mimi namuomba Rais Magufuli kama anavyosaidia mengine kwa wepesi, kwenye sanaa uweke mkono wako Baba tunakutegemea.” – Diamond.
Baada ya Diamond kuyaomba hayo, Rais Maguli alipiga simu moja kwa moja kwenye kipindi hicho na kusema:>>> “Nimemsikia Diamond na maombi yake nimeyapokea kwa mikono miwili nimefurahi kumskia siku ya leo natafuta siku ambayo tutakaa pamoja, nasikilizaga nyimbo zako hata wale wanaoigiza nawapenda sana na SHILAWADU.” – Rais Magufuli.
.>>> “Hongera sana Diamond hongera sana kuwa na watoto, wakati wa kampeni ulikuwa na mtoto mmoja sasa una wawili.“
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment