MAMA Mlezi wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Bi. Nuru Khalfan Kikwete, aliyefariki asubuhi jana asubuhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa matibabu, amezikwa leo katika makaburi ya Mwanakarenga, Bagamoyo, Pwani.
Rais Mstaafu Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akimpokea Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohudhuria mazishi ya Bibi. Nuru Halfan Kikwete ambaye ni mama mdogo wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne mheshimiwa Dk. Jakaya Kikwete nyumbani kwa marehemu Bagamoyo mkoani Pwani leo Machi 8, 2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki ibada ya kuuombea mwili wa marehemu Bibi. Nuru Halfan Kikwete ambaye ni mama mdogo wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne mheshimiwa Dk. Jakaya Kikwete nyumbani kwa marehemu Bagamoyo mkoani Pwani leo Machi 8, 2017. Kulia ni Rais Mstaamu Dk. Kikwete (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments :
Post a Comment