Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, April 6, 2017

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AWATAKIA HERI SERENGETI BOYS!

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wakati wa hafla fupi ya chakula cha usiku ambapo aliwaalika kwenye makazi yake timu ya Taifa ya Vijana (Serengeti Boys) kwenye makazi yake Oyster Bay, Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa hafla fupi ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa timu ya Serengeti Boys,jana usiku tarehe 04, Aprili 2017, Oyster Bay jijini Dar es Salaam.


Nahodha wa timu ya Serengeti Boys akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake mbele Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) wakati wa hafla fupi ya kuwatakia heri Serengeti Boys ambao wanajiandaa na fainali ya Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 yanayotarajiwa kufanyika Nchini Gabon.
Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni kwa timu ya Taifa ya Serengeti Boys iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Ally Hapi akitoa neno la shukrani kwa timu ya Serengeti Boys ambao walialikwa kwenye hafla maalum ya chakula cha jioni na Makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye makazi yake Oyster Bay, jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihudumu chakula kwa nahodha wa Serengeti Boys Issa Abdi Makamba wakati wa hafla fupi ya chakula cha jioni ambapo aliwaalika kwenye makazi yake timu ya Taifa ya Vijana (Serengeti Boys) kwenye makazi yake Oyster Bay, Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja wachezaji wa timu ya Taifa ya Vijana (Serengeti Boys) mara baada ya kula nao chakula cha jioni ambapo aliwaalika kwenye makazi yake Oyster Bay, Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na wachezaji wa Serengeti Boys mara baada ya kula nao chakula cha jioni ambapo aliwaalika kwenye makazi yake Oyster Bay, Dar es Salaam.

No comments :

Post a Comment