Morogoro. Jeshi la polisi mkoani hapa linamshikilia, mkazi wa kijiji cha Mamvisi Gairo kwa tuhuma za kumuua mke wake kwa kumpiga ngumi na mateke sehemu mbalimbali za mwili na kusababisha kifo chake.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amesema lilitokea Mei 22 mwaka huu saa 1.00 asubuhi katika kijiji cha Mamvisi, Wilayani Gairo.
Matei amesema baada ya kufanya mauaji hayo mtuhumiwa aliutupa mwili wa marehemu huyo kwenye mto Chumvi uliopo Gairo kwa lengo la kupoteza ushahidi.
Inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni baada ya marehemu kumuomba mtuhumiwa fedha za kumpeleka mtoto wao hospitali kufuatia maradhi aliyokuwa akiugua.

/Mwananchi.
No comments :
Post a Comment