Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, May 15, 2017

Godbless Lema: kuwa mpinzani Tanzania inahitaji uvumilivu!

Mbunge Godbless Lema amedai kuwa mpinzani wa siasa za bongo ni kazi ngumu sana, Mh Lema amesema hayo baada ya baaadhi ya watu kumdhihaki alipotoa shukrani zake kwa Mbunge Lazaro Nyalandu kufuatia kuwasaidia majeruhi wa ajali ya basi la Lucky Vicent.

Jana baada ya Mbunge Godbless Lema kumshukuru Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM) Lazaro Nyalandu kuna kundi la watu liliibuka na kuanza kutoa maneno ya dhihaka kwa Lema huku wengine wakipongeza na kusema ni jambo la kheri kwa mbunge huyo kutambua kazi iliyofanywa na Nyalandu, lakini baada ya mijadala hiyo kuzidi kuwa mikuba aliibuka Mh. Lema na kutoa kauli hii kumjibu mtu mmoja ambaye alikuwa akimdhihaki."Kuwa mpinzani wa siasa Tanzania ni kazi ngumu sana, ila hatukati tamaa kwa sababu upendo wetu ni mkuu kuliko dhihaka. Mungu akubariki" aliandika Godbless Lema



No comments :

Post a Comment