Waziri wa ujenzi mawasiliano na usafirishaji Balozi Ali Karume amewataka wafanyakazi na wahandisi wa wizara hiyo kushirikiana katika kufanya uchambuzi na utafiti wa kina ili kuangalia mapungufu yaliyojitokeza katika miundo mbinu ya barabara kisiwani Pemba kwa lengo la kuepusha uharibifu kwenye miundombinu hiyo.
Amesema wizara ipo kwa kufanya kazi kwa vitendo hiyo waendelee na nguvu waliyonayo katika kuihudumia jamii kwa kurejesha mawasiliano ya barabara pale yanapoharibikaBalozi Karume ameyasema hayo katika kikao cha pamoja cha wahandisi wa wizara ya ujenzi mawasiliano na usafirishaji cha kutathmini utendaji wa wizara katika kurejesha huduma ya miundo mbinu ya barabara na madaraja yaliyoharibiwa na mvua kisiwani Pemba.
Katika kikao hicho Katibu Mkuu wa wizara ya ujenzi Mawasiliano na miundo mbinu Mustafa Aboud Jumbe amewapongeza wahandisi hao kwa kuirudisha huduma ya mawasiliano kwa muda mfupi na wananchi kuweza kuendelea na shughuli zao za kawaida .
Hata hivyo amelaumu ni kwa nini barabara zilizojengwa zimeharibika kabla ya miaka mitano na kuwapa muda wahandisi hao hadi Ijumaa kuelezea kwa kitaalamu kitu cha kufanya cha kurudisha mawasiliano kutoka katika sehemu zilizoharibika.
Naye Afisa Mdhamini wa wizara ujenzi Mawasiliano na usafirishaji Pemba Hamad Ahmed Baucha na muhandisi wa wizara hiyo wameahidi kuyafanyiakazi maagizo hayo kwa kuhakikisha wanayasimamia na kazi inaendelea kama ilivyopangwa.
/ Pemba News
No comments :
Post a Comment