dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, May 20, 2017

KWA HILI MKUU WA MKOA WA ARUSHA MHE MRISHO GAMBO UNAFAA UTUMBULIWE. SIASA ZA KIJINGA ZITATUREJESHA NYUMA BAADA YA KUTUPELEKA MBELE. YOU MIS-USED AND ABUSED THE POWER BESTOWED UPON YOU BY WANANCHI!!!


Meya Arusha afunguka haya

Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro amesema kuwa ataelekeza fedha zote za rambirambi kwa wafiwa  badala ya kuzipeleka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Aidha amehoji ni kwanini fedha za rambirambi zilizochangwa kwaajili ya msiba wa wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja kuchotwa Sh.milioni 1.5 kupelekwa kama rambirambi katika msiba wa bwana na bibi harusi waliosombwa na maji Kata ya Sambasha iliyopo Wilayani Arumeru kama pole.


Meya, Lazaro aliyasema hayo leo Jijini hapa wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuachiliwa na Jeshi la Polisi leo majira ya saa 12:30 asubuhi kisha kwenda ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini.

Amesema fedha hizo za rambirambi zitakazochangwa na watu mbalimbali kisha kuletwa kwake kama Meya wa Jiji la Arusha, atazielekeza kwa wafiwa moja kwa moja badala ya kwa RC Gambo kwani RC huyo anaonekana kutumia fedha hizo kwa malengo mengine na kumtuhumu kuwa anachukua fedha zinazochangwa na kupeleka kwenye misiba ambayo ilitokea kipindi cha nyuma kama rambirambi.

Amesema wafiwa wanahoji ni kwanini fedha zilizobaki zilazimishwe kujenga  jengo la Wagonjwa Mahututi (ICU) Sh,milioni 56 huku akijua kabisa fedha hizo zimechangwa kwaajili ya rambirambi kwa wafiwa.

“Yani hili jambo ni la ajabu sana nimefika shuleni kutoa rambirambi na si mimi bali nimewasindikiza umoja wa shule binafsi na nikaomba viongozi wa dini wafanye sala kwaajili ya kuanza kutoa fedha hizo lakini cha ajabu nakamatwa kwa kosa gani ,na mimi nasema sitaelekeza fedha kwa RC Gambo ambazo ni za rambirambi bali zikija kupitia ofisi yangu nitazielekeza kwa wafiwa ambao wapo kwenye kila Kata,” alisema.

Naye  Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa alisema tukio lile ni tukio la aibu na wakati Fulani walimshauri RC Gambo awe mtu mzima akiendelea na mambo haya hatafika mbali.

Awali jana Mei 19, 2017, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo wakati akipokea msaada uliochangwa na wananchi kupitia tovuti ya  wezesha sasa ambapo alipokea msaada wa takriban shilingi milioni 4 alisisitiza kuwa wanasiasa waache kutumia msiba kwa kuingiza siasa kwani hakuna fedha yoyote ile iliyoliwa na pia wapo katika harakati za kuwatumia fedha wazazi pamoja na timu ya wataalam wa afya walioongozana na watoto wa Lucky Vicent ambao ni majeruhi wanaotibiwa nchini Marekani kama fedha za kujikimu na kiasi kilichobaki hadi sasa ni  zaidi ya Sh, milioni 56 ambazo kunakamati ndogo ya wazazi iliyoteuliwa ambao wataamua zitumikeje kwaajili ya kumbukumbu za watoto hao.
GAMBO AZUNGUMZIA SIASA TUKIO LUCKY LA VINCENT



Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo
By Moses Mashall, Filbert Rweyemamu mwananchipapers@mwananchi.co.tz
Arusha. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema kuwa tukio la msiba wa wanafunzi wa Lucky Vincent uliotokea hivi karibuni halikutegemewa na halipaswi kutumika kujinufaisha kisiasa, huku Meya wa Jiji la Arusha akiendelea kushikiliwa na polisi.

Meya huyo, Kalist Lazaro; viongozi wa dini na baadhi ya viongozi wa Shirikisho la Umoja wa Wamiliki wa Shule Binafsi Kanda ya Kaskazini (Tamongsco) wanashikiliwa na polisi baada ya juzi kukamatwa walipokwenda kutoa rambirambi katika shule hiyo.

Akipokea rambirambi kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwamo taasisi ya Wezesha Sasa walitoa Sh4.4 milioni, Umoja wa Wauza Mafuta Rejareja (Tapsoa) na Shule ya Dar es Salaam Independent (DIS), Gambo alisema jana kuwa kila mchango uliopokelewa utatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na hakuna pesa itakayopotea.

“Tusiangalie waliofiwa tu lakini tunapaswa tuangalie na hawa wanafunzi watatu walionusurika Mungu ana mipango nao na lazima tufanye jambo kwao kwa sababu nao ni sehemu ya waliohusika katika ajali iliyopoteza maisha ya watu 35,” alisema.

Alisema kelele zinaendelea juu ya matumizi yasiyo sahihi ya fedha zote zilizochangwa hazina msingi kwa sababu wakati kuna watu waliahidi, lakini hawakutoa kwa wakati na shughuli zisingeweza kusimama na Serikali ilitumia busara kutafuta fedha ili shughuli za kusafirisha miili na mazishi inafanikiwa.

No comments :

Post a Comment