Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Aziz P. Mlima akizungumza kwenye kikao cha Wataalamu ngazi ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam. Mkutano huu ni maandalizi ya Mkutano wa 34 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki unaotarajiwa kufanyika tarehe 18 Mei, 2017 Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama Bw. Stephene Mbundi akisisitiza wakati wa Mkutano wa ngazi ya Wataalam kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam
Sehemu ya wajumbe wakifuatilia mkutano
Katibu Mkuu Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Liberat Mfumukeko akifuatilia Mkutano.
No comments :
Post a Comment