JUMUIYA ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Wakulima Zanzibar, imekabidhi Sh. milioni 4.6 zikiwa ni msaada kwa watu walioharibikiwa na nyumba kutokana na mvua za masika zinazoendelea.
Fedha hizo zimetolewa kwa wananchi wa Shehia za Mbuyuni na Changaweni, Wilaya ya mkoani Pemba ambazo zitasaidia kufanya matengenezo nyumba zao.
Akikabidhi msaada huo kwa waathirika hao, Rais wa Jumuiya hiyo,Taufik Salum Turki, aliwataka waendelee kuwa na subira katika kipindi hiki.
Alisema jumuiya hiyo itashirikiana na Serikali ya Zanzibar ili kuhakikisha wananchi wanarudi katika hali zao za kawaida, ikiwamo kupata makazi.
“Hii ni mitihani ya Mungu, hivyo msiwe wa unyonge na kujihisi kuwa mmeonewa kwa kupata maafa haya, jambo la msingi ni kuendelea kuvumilia na mtapatiwa misaada ili muweze kurejea katika makazi yenu,” alisema.

No comments :
Post a Comment