Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) alipokuwa akiangalia jengo la ZSTC Mkoani Pemba lililoanguka ukuta kutokana na kuangukiwa na mti baada ya mvua kubwa za masika zilizonyesha hivi karibuni na kusababisha uharibifu mkubwa alipofanya ziara maalum leo (kushoto) Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe, Amina Salum Ali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto) alipofika kijiji cha Gando kumfariji na kumpa pole Mzee Juma Mjaka Khamis (kulia) akiwa na Familia yake aliyepata maafa ya nyumba yake kuangukiwa na mti na kupelekea kukosa sehemu ya kuishi baada ya mvua kubwa za masika zilizonyesha hivi karibuni kisiwani humo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba Mhe,Hemed Suleiman alitembelea Kijiji cha Makombeni Wilaya hiyo kuangalia nyumba mbali mbali za Wananchi zilizopatwa na athari zilizotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha kisiwani humo leo wakati alipofanya ziara maalum ya kikazi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (katikati) alipofika katika daraja la Chamanangwe leo kisiwani Pemba lililokatika kutokana na maji ya Mvua zilizonyesha hivi karibuni na kusababisha usumbufu kwa wanaotumia daraja hilo kutoka upande mmoja kuelekea sehemu nyengine wakati alipofanya ziara maalum ya siku moja ya kikazi (Picha na Ikulu).
No comments :
Post a Comment