Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, May 15, 2017

Zitto Kabwe asikitishwa na kitendo alichofanyiwa Adam Malima, atoa kauli!

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zuberi Zitto Kabwe amesikitishwa na kitendo kilichofanywa na moja ya askari polisi kumtishia bunduki aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima

Zitto kabwe ameonyesha masikitiko hayo kupitia ukurasa wake wa kijamii Facebook akihoji kama polisi wanafundishwa kuwafanyia hivyo raia.

"Hii ni nini ?, askari wetu wanafundishwa kufanya hivi, Waziri Mwigulu huyu yupo wazi na ni wa kutoka kwako. Unahitaji uchunguzi". Ameandika Zitto.
Zitto ameandika hayo baada ya masaa machache kupita kwa tukio hilo lililowahusisha askari hao walioambatana na kampuni ya Majembe Auction Mart waliokuwa wakitaka kujaribu kukamata gari iliyokuwa imeegeshwa pembeni ya barabara ya Masaki karibu na Hoteli ya Double tree ingawa ndani ya gari hilo alikuwepo dereva.


No comments :

Post a Comment