Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Rufiji, Onesmo Lyanga.
Kwa mujibu wa wauguzi hao, walioomba hifadhi ya majina yao kwa kuhofia usalama wao, kitendo cha kuwaweka majeruhi hao hospitalini hapo ni hatari kwao na hata wahudumu wenyewe, endapo wauaji hao wataamua kwenda kuwamalizia baada ya kuwakosa huko majumbani.
“Hawa watu wanafanya mauaji kwa malengo ambayo hayafahamiki, sasa tunahofia ipo siku watataka kuja kuwamalizia hapahapa, sijui itakuwaje maana hata sisi sasa tuna hofu kubwa sana, hatuna ulinzi kwa hiyo wakija watatuokota tu kama kuku,” alisema muuguzi huyo.
Licha ya kilio cha usalama wao, pia wauguzi hao walisema kitu kingine kinachowapa tabu ni kukosekana kwa mawasiliano ya simu, kwani eneo hilo halina ‘network’ kwa muda mwingi.
Akizungumzia hilo, mmoja wa wauguzi hao alisema licha ya eneo hilo kuwa na wakazi wengi wanaohitaji huduma ya mawasilino ya simu, lakini hali ni ngumu sana.
“Sasa kwa mfano hata kama wakija hapa hao wahalifu, itachukua muda mrefu sana kupata msaada kwa sababu hatuwezi kupiga simu kwa wakati.
“Inafikia wakati tunataka kumpa mgonjwa rufaa ya kuelekea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili au hospitali nyingine, lakini tunashindwa kufanya mawasiliano na huko tunakotaka kumpeleka.
“Wakati mwingine tunahitaji kutuma nyaraka mbalimbali za kikazi kupitia mitandao au kwa kuwasiliana na madaktari wa sehemu nyingine, lakini hilo nalo linakuwa gumu kwa ajili ya kusaidiana mawazo lakini hilo nalo linakwama.
“Tunaziomba kampuni za simu zituletee huduma huku jamani, maana hata ukiachana na hii hospitali huku kuna watu wengi wanaohitaji huduma ya mtandao,” alisema muuguzi huyo.
Vitendo vya mauaji ya raia na viongozi wa vijiji na serikali za mitaa vinaendelea kutikisa katika Wilaya za Kibiti, Rufiji na Mkuranga mkoani Pwani na hivyo kuwa tishio kubwa kwa wananchi.
/ Global Publisher
No comments :
Post a Comment