dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, July 27, 2017

Mganga wa jadi achomwa mkuki mgongoni!

WATU watano wakiwemo watoto wawili wamekufa katika matukio tofauti yaliyotokea mkoani hapa hivi karibuni ambapo mganga wa jadi, Levocatus Kanjalanga (65) aliuawa kikatili kwa kuchomwa mkuki mgongoni na mtu asiyefahamika.

Matukio hayo ambayo yametokea katika Wilaya za Nkasi, Kalambo na Manispaa ya Sumbawanga yamethibitishwa kwa nyakati tofauti na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, George Kyando (pichani) na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Said Mtanda.

Mtoto wa mganga huyo, Simon Kanjalanga alilieleza gazeti hili kuwa baba yake aliuawa juzi saa moja na nusu asubuhi kwa kupigwa na mkuki mgongoni akiwa anatembea mitaani katika kitongoji cha Chawe kilichopo katika Mji wa Namanyere wilayani Nkasi.Taarifa kutoka eneo hilo la tukio zinaeleza kuwa mganga huyo wa kienyeji alikuwa akituhumiwa na wateja wake kuwa alikuwa akiwatoza fedha nyingi za matibabu lakini walikuwa hawaponi kupitia uganga wake huo.

Akithibitisha Mkuu wa Wilaya hiyo, Mtanda alieleza kuwa watu wawili wameuawa kikatili wilayani humo akiwemo mganga huyo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni imani za kishirikina .

No comments :

Post a Comment