Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, July 27, 2017

USA: Mahakama yaamuru Marehemu Michael Jackson kumlipa Quincy Jones Sh20.7 bilioni!

Mtayarishaji nguli wa muziki, Quincy Jones ameshinda kesi ya madai ya Dola za Marekani 9.4 milioni (sawa na takriban Sh20.7 bilioni za Kitanzania) ikiwa ni mrabaha na ada ya kurekodi kazi za aliyekuwa mfalme wa pop duniani, Michael Jackson, magazeti ya Marekani yameripoti.

Jones alifungua kesi hiyo mwaka 2013 akidai Dola za Marekani 30 milioni, lakini Kampuni ya Michael Jackson ikasema kuwa mtayarishaji huyo alikuwa akidai Dola za Marekani 392,000 pekee.

Wiki iliyopita, Jones ambaye anasifika kwa kutayarisha albamu kama “Thriller”, Of The Wall” na “Bad” alisema wakati wa kutoa kiapo kuwa alidanganywa na kuwekwa kando katika mpango wa kutengeneza fedha nyingi, kwa mujibu wa tovuti ya AP.Baada ya kifo cha Michael Jackson, kampuni iliweka nakshi (remix) nyimbo zake bila ya kumshirikisha Jones ili asistahili malipo ya mrabaha kutokana na nyimbo hizo.

“Mfano mmoja ni filamu ya ‘This Is It,'” alisema Jones. “Jina langu halipo sehemu yoyote karibu na huo wimbo.”

Henry Gradstein, mmoja wa wanasheria wa Jones, alisema Weitzman hakuielewa mikataba ya Jones.

“Mikataba inaeleza kuhusu malipo ya leseni,” alisema. “Kwa miaka 35, pande hizo mbili zimetafsiri kwa njia hiyo na kulipa kwa misingi hiyo. Kusema kwamba ilikuwa zawadi, ni fedheha.”

Tovuti ya Billboard imekariri Jones akisema hukumu hiyo ni ushindi kwa sanaa.

"Kesi hii haikuwa kwa ajili ya Michael, ilikuwa ni kulinda heshima ya kazi tuliyofanya wote katika kurekodi muziki na kumbukumbu ya tulichobuni,” alisema nguli huyo aliyetayarisha wimbo maarufu wa “We Are The World”.

“Ingawa hukumu hii haijatoa kiwango chote tulichodai, nina furaha kwa sababu uamuzi umetunufaisha katika hili. Naungalia ushindi huu si kwa ajili yangu pekee, bali wasanii kwa ujumla.”

No comments :

Post a Comment