Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, July 30, 2017

Uturuki yaomba msaada Tanzania!

Image result for turkish flag
Tanzania imeombwa kuisaidia Uturuki kiwango cha Tani 20 ya Korosho kufuatia nchi hiyo kuwa na uhaba mkubwa wa bidhaa hiyo yenye uhitaji zaidi nchini Uturuki.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara kutoka Uturuki ijulikanayo kama 'Turkish Exportetrs Assembly' (TIM) Bwana Kemal Batuhan Yazici amesema kuwa, kiwango cha korosho kilichopo nchini kimeshuka wakati mahitaji ya nchi ni Tani 20, hivyo wanaitegemea Tanzania kuondoa uhaba huo nchini mwao.Kemal Batuhan Yazici amesema, Korosho inayohitajika nchini Uturuki ni ile ambayo tayari imechakatwa na kufungwashwa vyema kwa viwango vya kimataifa na sio malighafi hivyo ni vyema wafanyabiashara hiyo wakaandaa utaratibu wa haraka kuhakikisha Korosho zinasafirishwa kutoka Tanzania kwenda nchini Uturuki.

Kwa muda wa miezi sita, kiwango cha biashara kati ya Tanzania na Uturuki kimeongezeka kwa asilimia 9 kwa bidhaa za Tanzania zinazosafirishwa kutoka nchini Tanzania kwenda nchini Uturuki hivyo ongezeko hilo linaashiria Tanzania kupata soko lenye tija nchini Uturuki.

Katika siku za hivi karibuni nchi ya Uturuki imeongeza ushirikiano wake wa kibiashara na nchi ya Tanzania ambapo nchi hizo zimepata fursa mara kadhaa kuonesha maeneo yao ya uwekezaji baina yao ili kuongeza faida na kuleta maendeleo.

No comments :

Post a Comment