Lipumba ameendelea kumtaka Katibu mkuu huyo arejee katika Ofisi yake ya Buguruni tena bila hata ya kuomba msamaha kwa Mwenyekiti wake, ingawa atalazimika kupokea maagizo ya kiutendaji kutoka kwa Mwenyekiti wake.
"Maalim analalamika lakini malalamiko yake hayana msingi, yeye ni Katibu Mkuu anapaswa kufuata misingi ya Mwenyekiti, anatambua kuwa Mwenyekiti ni boss kwa mujibu wa Katiba ya CUF, Mwenyekiti nipo yeye aje kufanya kazi hapa. Maalim ni mkongwe wa siasa tunataka kuwa na maelewano, nampigia simu hapokei, nasikia saizi akija Dar es Salaam anakwenda uchochoroni huko Magomeni wakati tuna ofisi hapa nzuri, Katibu Mkuu unauzoefu wa kisiasa tufanye majadiliano ofisi zetu ziko hapa njoo tuzungumze" Alisema Lipumba
No comments :
Post a Comment