dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, August 7, 2017

Mbunge wa Lindi atema Cheche kuhusu ubunge wake!

Na. Ahmad Mmow, Lindi.MBUNGE wa Lindi mjini, Hassan Kaunje, amesema yupo tayari kunyimwa kura katika uchaguzi mkuu ujao, iwapo nilazima awe muongo na mwenye ujuzi wa kugeuza maneno. Kaunje aliyasema hayo,jana alipozungumza na wananchi wa mtaa wa Mikumbi, manispaa ya Lindi.

Mbunge huyo anayetokana na  CCM alisema kwa muda mrefu katika jimbo hilo utendaji wa mbunge unapimwa kwa namna anavyowexa kubadili maneno na kuwalaghai wananchi kwa ahadi tamu na mzuri zisizo tekelezeka.
"Aya ninayo Sema yanaweza kuwa sio ya kawaida kuyasikia nasio mazuri kwa baadhi ya watu . Lakini nilazima niseme, kwasababu imezoeleka ukiwa mbunge uwe umauwezo wa kugeigeuza maneno, kuishambulia serikali na kuwashambulia wanachama na viongozi wa vyama vingine na kukashifiana. Niweke wazi kwamba kama hizo ndizo sifa za kuwa mbunge sahihi anaetakiwa kuongoza jimbo hili basi naomba nisipewe kura nikiomba tena, "alisema Kaunje.Mbunge huyo ambae alitumia mkutano huo kueleza utekelezaji wa ahadi mbalimbali ambazo alihaidi wakati anaomba kuchaguliwa kwa kwanafasi hiyo. Alisema sifa ya kiongozi sio ufundi wa kukashifu wengine au kupinga kila jambo linalofanywa na watu wenye itikadi tofauti ya vyama vya siasa. Bali kuyapokea na kuwafanyia kazi mawazo ya kimaendeleo bila kujali aliyetoa wazo hilo au anayetenda ni wachama kingine.
"Hali hii inasababisha mtu wa CCM kushindwa kupokea ushauri na kufanyia kazi mawazo mema ya upande mwingine. Nawaupande mwingine kupinga kila kitu kinachofanywa na serikali au kiongozi anayetokana na CCM, hatuwezi kufika kokote tukiendekeza siasa za aina hiyo, "alisema.

Katika kuonesha yupo tayari kufanyakazi na kushirikiana na yeyote katika shuguli za maendeleo katika jimbo hilo, mbunge huyo alisema nijambo la ajabu kuona  wananchi wanatengana na kuhasimiana kwasababu za itikadi za siasa, wakati Rais Dkt John Magufuli anaendelea kuwateuwa viongozi na watendaji katika serikali anayoingoza kutoka nje ya CCM ili kujenga umoja. Japokuwa ni mwenyekiti wa chama hicho.

Mbali na hayo Kaunje aliwashukia wanaCCM wenzake kwakuwaambia hataki kushiriki kupanga safu ya uongozi ndani ya  chama kupitia chaguzi za ndani za chama hicho. "Wala msitarajie kama kuna mtu nitamsaidia ili ashinde nafasi ya uongozi ndani ya chama kama ilivyozoeleka na watu wengine ili kujitengenezea mazingira ya uchaguzi mkuu ujao. Wewe pambana mwenyewe,mwanachama atakae chaguliwa nitashirikiana nae," alisema Kaunje.

Mbunge huyo ni miongoni mwa wabunge wanne wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi, kati ya  nane wa kuchaguliwa waliopo katika mkoa huu wa Lindi. Wabunge wanne wengine  wanatokana na CUF- Chama Cha Wananchi. 

No comments :

Post a Comment