dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, August 7, 2017

MWALIMU ATIWA MBARONI KWA KUFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI WAKE WA KIDATO CHA NNE!

Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Igurubi, Maganga Ngassa (35) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Igunga kwa tuhuma ya kufanya mapenzi na mwanafunzi wa miaka 17 anayesoma shule ya sekondari kidato cha nne, Kata ya Mwisi wilayani hapa.

Mwendesha Mashitaka wa Polisi Igunga, Elimajid Kweyamba alidai mbele ya Hakimu Juhudi Mdonya, kwamba Julai 25, mwaka huu saa 9 alasiri katika nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Forest au Chacha iliyoko Mtaa wa Mwayunge mjini Igunga, kinyume na sheria za nchi, Ngassa alifanya mapenzi na mwanafunzi  mwenye umri wa miaka 17 anayesoma shule ya sekondari iliyoko Kata ya Mwisi kidato cha nne (jina linahifadhiwa). 

Mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 18, mwaka huu itakapotajwa tena.

No comments :

Post a Comment