Wafuasi wa chama tawala nchini Afrika Kusini wakifurahi baada ya kura ya kutokuwa na imani dhidi ya rais Zuma kushindwa.
Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma ameponea kura ya kutokuwa na imani naye bungeni baada ya wabunge wengi wa chama tawala cha ANC kumuunga mkono.Jumla ya wabunge 177 walipiga kura ya kumuondo madarakani rais Zuma huku wabunge 198 walipiga kura ya kumuunga mkono.
Wabunge tisa hawakupiga kura.
Wafuasi wa rais Jacob Zuma walishangilia ushindi huo kupitia vigelegele na kucheza densi.
Wabunge 40 wa chama tawala cha ANC walipga kura ya kutaka kumng'atua mamlakani alisema mwandishi wa BBC Milton Nkosi kupitia ujumbe wake wa Twitter.Chama cha upinzani nchini humo Democratic Alliance kinasema kuwa wabunge wengi wa chama tawala cha ANC walipiga kura hiyo wakizingatia maswala ya ufisadi.
Lakini ushindi wake ulikuwa mdogo , ikimaanisha kwamba idadi kubwa ya wabunge kutoka chama tawala cha ANC iliunga mkono muswada huo wa upinzani kumuondoa madarakani.
Waziri wa polisi nchini humo Fikile Mbalula ameamewataja wabunge wa chama tawala waliounga mkono kura hiyo kuwa wauawaji wa kujitolea muhanga.
''Kwa nini munataka kumng'oa rais Zuma?'',aliuliza.
Bwana Mbalula alikuwa akiwahutubia wafuasi wa chama cha ANC nje ya bunge muda mfupi baada ya kura hiyo kushindwa.
No comments :
Post a Comment