Wafanyakazi wa Shirika la Bandari Zanzibar wakiwa katika harakati za kuupakia Waya wa Umeme kwa ajili ya kusambaza huduma ya Umeme katika Kisiwa cha Fundo Kisiwani Pemba ili kuwawezesha kupata huduma hiyo kwa maendeleo yao. Umeme huo utapita baharini ukuitokea katika Kijiji cha Ukunjwi Wilaya ya Wete. Umeme huo utavinufaisha vijiji vinne vilioko katika kisiwa hicho na taratibu za kuweka waya na nguzo katika kisiwa hicho tayari zimeshakamilika kinachosubiriwa ni utandandazaji wa waya huo ulioagizwa kutaka Nchini China na una uwezo wa kuchukua KV 33.utapita baharini haki katika kisiwa hicho.
Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar akiukagua waya huo kabla ya kupakiwa katika Meli ya MV Jituihadi kuaza zoezi hilo la utandikaji wa wayo huo utakoofanywa na mafundi wa Shika la Umeme Zanzibar ZECO hadi kisiwani humo. Kazi hiyo inatarajiwa kuchukuwa siku tano hadi kukamilika kwake nu kutowa fursa za utumiaji wa Umeme huo kwa Wananchi wa Kisiwa hicho. kwa mujibu wa taarifa ya Meneja Mkuu wa ZECO.
/ Mapara
No comments :
Post a Comment