Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akihojiwa na Joseph Msami wa Umoja wa Mataifa baada ya kushiriki kikao cha ngazi ya juu wiki ya Afrika kilichoangazia masuala ya miundombinu na kilimo. (Picha:Idhaa ya Kiswahili/Assumpta Massoi)
Rais mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete amesema uchangishaji fedha kwa ajili ya miundombinu na kilimo ni lazime uende pamoja kwa sababu masuala hayo ni mtambuka.
Kikwete amesema hayo akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani baada ya kushiriki kikao cha ngazi ya juu cha Wiki ya Afrika ambapo masuala ya tabianchi, miundombinu, kilimo na vijana yameangaziwa.
Amesema uchangishaji usiotosheleza wa fedha katika sekta ya kilimo unakwamisha wakulima kushiriki kilimo cha kisasa akitoa mfano akisema…
(Sauti ya Kikwete)
Kikwete amesema miundombinu bora kama vile barabara, reli, viwanja vya ndege ni viwezeshaji vya ukuaji wa uchumi kwa kuwa hurahisisha usafirishaji wa mazao ya kilimo na
No comments :
Post a Comment