Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, October 19, 2017

Ninatafakari uwezekano wa kushiriki uchaguzi - Odinga!

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amesema, anaweza kubadilisha mawazo na kurejea kwenye kinyanganyiro cha kuwania urais iwapo kutakuwa na mazungumzo na kufanyika kwa mageuzi ndani ya Tume ye Uchaguzi.

Odinga ametoa kauli hii baada ya kukutana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi jijini Nairobi.

Mkutano huu umekuja baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Wafula Chebukati hapo jana kuomba mazungumzo ya moja kwa moja kati ya rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga.

Hata hivyo, mkutano huo haujafanyika kama ilivyokuwa imepangwa na baada ya Odinga kuzungumza na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, amemwambia kuwa atakutana na rais Kenyatta siku ya Jumatatu.Uhuru Kenyatta kwa upande wake, akiendelea na kampeni za kisiasa amesema kuwa mazungumzo pekee anayoweza kushiriki ni kuhusu namna Uchaguzi wa wiki ijayo utakavyofanyika kwa amani.

Hii ni dalili kuwa huenda mwafaka usipatikane hivi karibu kuhusu Uchaguzi wa tarehe 26.

Odinga ameitisha maandamano ya nchi nzima siku ya kupiga kura, hali ambayo imeendelea kuzua wasiwasi.

Wachambuzi wa siasa wameendelea kutoa wito wa kufanyika kwa mazungumzo na kuahirsihwa kwa Uchaguzi huu kwa sababu tayaru Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi amesema, itakuwa ni viumu kuwa na uchaguzi huru na haki katika mazingira haya. Wito kama huu umetolewa na mashirika ya kiraia nchini humo.

No comments :

Post a Comment