Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, October 7, 2017

RAIS MAGUFULI AFANYA MABADILIKO KATIKA BARAZA LA MAWAZIRI, WANNE WATEMWA!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitangaza mabadiliko madogo katika baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 7, 2017. Wakimsikiliza ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi pamoja na maafisa waandamizi wa Ofisi ya Rais. Picha na Ikulu

Rais John Magufuli amefanya mabadiliko ya baraza la mawaziri kwa kuwatema mawaziri wanne waliokuwepo kwenye baraza la awali.
Mawaziri walioachwa ni aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe na nafasi yake kuchukuliwa na Hamis Kigwangwala aliyekuwa Naibu Waziri Wizara ya Afya.
Mwingine aliyeachwa ni aliyekuwa Waziri Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge ambaye nafasi yake imechukuliwa na Mbunge wa Katavi, Mhandisi Issack Kamwele aliyekuwa naibu waziri wa wizara hiyo.
Panga hilo limempitia pia aliyekuwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura ambaye nafasi yake imechukuliwa na Mbunge wa Viti Maalum CCM, Juliana Shonza.
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani naye ametupwa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga.
Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kufanya mabadiliko ya baraza lake la mawaziri tangu aingie madarakani.

List ni kama ifuatavyo:
Utawala bora Mkuchika
Tamisemi Jafo
Mazingira-Makamba/Lugola
Kazi/vijana-Mhagama/mavunde/Stella Ikupa
Kilimo-John Tizeba/Mary chuki mwanjelwa
Uvuvi-Mpina/Abdala Ulega
Mawasiliano-Mbarawa/Elias kuandikwa
Fedha/Mipango-No change
Nishati-Kalema/Subira mgwalu
Katiba sheria-Kabudi
Mambo ya nje-Augustino Mahiga/Kolimba
Ulinzi-Mwinyi
Mambo ya ndani- Mwigulu 
Maliasili utalii-Khamis kigwangala/Josephat gasunga
Ardhi-Lukuvi/mabula
Viwanda- no change/many any
Elimu- no change/ole nasha
Habari/utamaduni-Mwakyembe/Juliana shonza

Katibu wa bunge-Stephen kagaigai. Kashirila atapangiwa Kazi nyingine

No comments :

Post a Comment