Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Friday, October 20, 2017
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein Amefanya Uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri, Usajili wa Magazeti na Vijarida Zanzibar!
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 4 (a) cha Sheria ya Usajili ya Magazeti na Vijarida Namba 5 ya Mwaka 1988, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, amemteua Bwana Yussuf Omar Chunda kuwa MWENYEKITI WA BODI YA USHAURI YA USAJILI WA MAGAZETI NA VIJARIDA, ZANZIBAR.
Uteuzi huo umeanza tarehe 19 Oktoba, 2017.
Taarifa ya uteuzi huu kutoka Ikulu Zanzibar, imesainiwa na Dkt. Abdulhamid Y. Mzee, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, ZANZIBAR.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment