Watu watatu wanaotuhumiwa kwa uhalifu wa mauaji ya Kibiti wamefariki dunia katika hospitali ya Temeke waliko kuwa wanafanyiwa matibabu baada ya kujeruhiwa kwenye majibizano ya risasi baina yao na Askari Polisi.
Akielezea kuhusu tukio hilo Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam SACP Lazaro Mambosasa amesema tukio hilo lilitokea Oktoba 16,2017 majira ya saa nne usiku maeneo ya Msongola Ilala.
“Askari wakiwa doria katika ufuatiliaji wa watuhumiwa wa mauaji ya Kibiti, waliona pikipiki ikiwa haina namba na ikiwa na watu watatu eneo la Barabara ya Mbande, katika kuwafuatilia pikipiki hiyo iliongeza mwendo na kukatisha njia kuingia Barabara ya vumbi,” amesema na kuongeza.
“Baada ya kugundua wanafuatiliwa na askari watu hao walianza kufyatua risasi hali iliyopelekea askari kujibu mashambulizi na majambazi hao wote kupigwa risasi na kuanguka chini na pikipiki yao, katika upekuzi watu hao walikuwa na Silaha aina ya SMG moja ikiwa imefutwa namba zake na magazine moja ndani yake kukiwa na risasi 16, maganda 10 ya SMG, mabomu aina ya Graned 7 na pikipiki moja aina ya Fekon nyekundu.”
Amesema majambazi hao hawakutambulika majina yao na kwamba juhudi za kutambua mtandao wa wahaalifu hao zinaendelea. Marehemu hao wanakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30-40. Miili yao imehifadhiwa katika Hospitali hiyo ya Temeke.
No comments :
Post a Comment